WAHANGA WA MKASA WA ST JOSEPH WAMALIZA SEMESTER BILA ''......
Mnamo tarehe 19 Feb 2016 tume ya vyuo vikuu ilifungia vyuo shiriki viwili vya Chuo kikuu cha Mt Joseph kutokana na kushindwa kutekeleza matakwa ya mkataba wa utoaji elimu hapa nchini Tanzania.
Kutokana na hatua hiyo ya serikali kuvifungia vyuo hivyo vishiriki ambavyo ni St Joseph University College of Agricultural science and Technology, Songea na St Joseph University College of Information Tehnology, Songea, ililazimika wanafunzi hao kuhamishiwa katika vyuo vikuu vingine ambavyo ni SUA, RUCU pamoja na UDOM.
Katika hali isiyokuwa ya kawaida,wakati vyuo vishiriki hivyo vikifungwa serikali kupitia TCU yaani Tanzania Commission of Universities iliahidi kuwa wanafunzi wangelipwa gharama zote za uhamisho jambo ambalo limegeuka kuwa kitendawili kisichojibika....Sambamba na hilo jambo linalotusikitisha sana uongozi wa Maramba media kama wadau wa elimu Tanzania ni kuwa tangu wanafunzi hao wahamishwe hadi wakati tukichapisha habari hii, zaidi ya wanafunzi 300 walio kati ya wanafunzi waliohamishiwa SUA hawajalipwa fedha zao za kujikimu kutoka HESLB ambayo ndiyo taasisi inayosimamia jambo hilo....Baadhi ya wanafunzi tuliohojiana nao wamedai kuwa hakuna majibu yoyote ya kuridhisha kutoka chuoni hapo wala HESLB......Kama wadau wa elimu Tanzania MARAMBA MEDIA tunapenda kutoa rai yetu kwa Waziri wa elimu Prof Joyce Ndalichako aweze kuliangalia jambo hili kwa mapana yake , pamoja na taasisi husika kwani pasipo hivyo Taifa litashindwa kufikia malengo.
No comments:
Post a Comment