Sunday, 10 July 2016

Kuelekea UE

UE KULETA NEEMA TZ
Mitihani ya vyuo vikuu Tanzania maarufu kama UE inatarajiwa kuanza hapo kesho tarehe 11 Feb 2016 kwa vyuo kadhaa nchini ikiwepo IFM, SOKOINE pamoja UDSM.....Ni siku chache zimepita tangu nchi ya Rwanda iahidi kuisaidia Tanzania wataalamu wa IT ili kufanikisha zoezi la ukusaji wa mapato TZ....
Maramba media imefanikiwa kufanya mahojiano na wanafunzi kadhaa ambao wapo mwaka wa mwisho wa masomo yao na wametoa maoni yao juu Rwanda kuisaidia TZ wataalamu...Wanafunzi hao wamesema Tanzania ya sasa sio nchi yenye shida ya wataalamu bali inahitaji mifumo rafiki na viongozi imara kisiasa na wenye UZALENDO kwani miradi mingi iliyowahi kufeli nchini chanzo ni kutokuwepo viongozi makini pamoja na sababu nyingine ndogondogo....Aidha wamefika mbali zaidi kwa kuishauri serikali ya awamu ya 5 kuweka misingi imara na kuajiri vijana wa kutosha kati ya wahitimu wa mwaka huu katika sekta zote ili kuongeza ufanisi wa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa kwani vijana wanakuwa na uzalendo wa kazi zaidi ya wazoefu wa muda mrefu,pia ndi muda ambapo wataweza kuibadilisha elimu walioipata kwenda katika uzalishaji.........
Pamoja na hayo, pia wamesisitiza kuwa gharama za kuazima wataalamu nje ya nchi kwa kazi ambazo zaweza kufanywa na wataalamu wa hapahapa nchini ni kupoteza akiba ya fedha za kigeni ambazo zingeweza kufanya kazi nyingine za kimaendeleo.....
Kwakuwa huu ni wakati wa Tanzania iliyosubiriwa kwa miaka mingi, ni matumaini yetu sisi Watanzania kuwa serikali itayafanyia kazi mawazo hayo ya vijana wasomi wazalendo wa Kitanzania.....
Maramamedia inapenda kuwatakia wanafunzi wote wa SUA, IFM, UDSM pamoja na vyuo vyote vikuu Tanzania maandalizi mema ya mitihani yao,pia inawakumbusha wale wanaotegemea kuhitimu kuwa...."BAADA YA KUTUMIA GHARAMA KUJIENDELEZA KITAALUMA, SASA NI WAKATI WA TAIFA KUNEEMEKA KUPITIA UTAALAMU MLIOUPATA"

No comments:

Post a Comment