Sunday, 10 July 2016

Janga

PIGO KUBWA LATOKEA SUA

 
Picha ya Wardat Jampan
(marehemu)

Miezi michache baada ya mwanafunzi wa kiume wa mwaka pili chuo kikuu cha Sokoine katika kozi Sayansi ya chakula kupoteza maisha akiwa amelala maeneo ya mazimbu, pigo lingine limewapata tena wanafunzi wa chuoni hapo baada ya kumpoteza binti Wardat Jampan mwanafunzi wa ngazi ya cheti katika kozi ya IT......Binti Wardat aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Mazimbu inayomilikiwa na Chuo hi alifikwa na umauti jioni ya tarehe 10 July 2017, ikiwa ni masaa machache kabla ya siku ya kuanza mitihani ya mwisho wa mwaka kufika......Mwili wa marehemu ulisafirishwa usiku wa siku hiyohiyo kweda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yatakayofanyika saa nne asubuhi kesho yake (Leo) tarehe 11/7/2016

Bwana alitwaa, Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe. Amina

No comments:

Post a Comment