Tuesday, 12 July 2016

UHARIBIFU DARAJA-KIGAMBONI


JE, UMEIKOSA VIDEO FUPI YA UHARIBIFU ULIOTOKEA BAADA YA LORI KUPINDUKA DARAJA LA KIGAMBONI?
 
Ilitokea ajali ya Lori lililokua na Kontena kwenye daraja la Nyerere Kigamboni Dar es salaam usiku wa kuamkia July 11 2016 ambapo ajali hiyo imesababisha majeruhi pamoja na eneo la barabara kuharibiwa, Meneja msimamizi kwenye hili daraja Gerald Sondo alipohojiwa kuhusiana na ajali hiyo alisema tangu daraja hilo maarufu kama Daraja la Nyerere kuanza kutumika hiyo ilikuwa ajali ya kwanza kubwa kuwahi kutokea katika daraja hilo. Ajali hiyo ilisababishwa na gari aina ya SEMI TRAIOLER iliyoacha njia yake na kuzigonga kingo za barabara mojawapo katika flyover (Mandela Road)
Gari hilo lilikuwa likitokea  maeneo ya kigamboni kuelekea mjini. Kutokana na kanuni na taratibu za usimamizi wa daraja hilo, Meneja msimamizi alisema kuwa Uongozi utafanya tathmini ya uharibifu ili matengenezo yaweze kufanyika, lakini pia akasisitiza kuwa baada ya taratibu za kiserikali na kipolisi kukamilika, mhusika aliyesababisha ajali hiyo atawajibika kulipia gharama zote za matengenezo.,,,,,...Tembelea link hapa nchini kwa maelezo zaidi
http://youtu.be/-Wa2GqzcIC4

No comments:

Post a Comment