Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania imejitokeza leo tarehe 16 July 2016 na kutolea maelezo kuhusu utata ulikuwepo kuhusu wakina nani wana sifa ya kusoma degree kwa mwaka wa masomo 2016/17.....
Kwa mujibu wa tangazo lilotolew kwa umma na Katibu mtendaji wa TCU hivi leo ni kuwa tofauti na ilivyoeleweka mara baada ya marekebisho ya vigezo vya kusoma shahada hapa nchini, kwamba ni lazima kupata D mbili ili udahiliwe sio sahihi.....
Kwa mujibu wa tangazo hilo, inatakiwa mhitimu wa kidato cha sita awe najumla ya point 4 katika masomo mawili kati ya matatu ya mchepuo aliosoma......Hivyo mtu aliye na Ufaulu wa C na E atasoma shahada....
Mchanganuo kwa mwaka 2013 kurudi nyuma na mwaka 2016 , A=5, B=4, C=3, D=2, E= 1
Kwa wahitimu wa mwaka 2014-2015, matokeo yao yalukuwa katika mfumo tofauti..Kwao A=A=5, B+=B=4, B=C=3, C=D=2, D=E=1..............Kwa sababu hii, ilivyohesabika awali kuwa ni lazima kuwa na D mbili ndio udahiliwe sio sahihi.....Kwa maelezo zaidi tembelea kiungo cha tovuti ya TCU hapa chini.
www.tcu.go.tz