20 September 2018 majira ya Saa nane alasiri iligeuka simanzi jijini Mwanza na viunga vyake.
Hii ni baada ya kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Buhorora Ukerewe na Ukara (visiwani) kupata ajali kikiwa kinakaribia kabisa kutia nanga.Imeelezwa kuwa kivuko hicho huenda kilibeba uzito zaidi ya uwezo wake kwani hata idadi ya maiti zilizookolewa ni zaidi ya 131 huku walio hai wakiokolewa takribani 40 + Injinia mmoja aliyeokolewa baada ya siku mbili (Sept 22)
Kinachoshangaza ni kuwa vyombo vya usafiri majini huwa na mstari mweusi au mwekundu ambao haupaswi kuzama wote majini.Mstari kama ungeangaliwa kabla ya safari kuanza huenda ungesaidia kuona kama uzito umezidi au la hasha.Bado haijabainika kama ukaguzi huo ulifanyika.
Ni vema pia katika karne hii ya sayansi na technolojia kukawekwa madaraja ya kupimia uzito/Weight bridge/Mizani katika bandari zetu kama Bado hatujafanya hivyo ili kupunguza uwezekano wa ajali za uzembe kutokea kutokana na ukadiriaji wa kizamani.
Mungu azilaze roho za marehemu wetu mahali pema peponi.Amina
Saturday, 22 September 2018
AJALI MV NYERERE MAJONZI MWANZA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment