Ikiwa zimepita siku 32 tangu kupotea katika katika namna isiyoeleweka kwa Mwanaharakati Ben Rabiu Wa Saanane mnamo Nov 18, 2016, hizi ni baadhi ya dhahania zilizopo katika mawazo ya Watanzania wengi.
Suala hili naligawanya katika matabaka 3 (yenye kujengwa na dhahania siyo uhalisia)., na matabaka hayo yote yana nguvu kubwa ya hisia hasi au chanya kuhusu sakata hili la ndugu yetu huyu.., nitafafanua matabaka ya fikra na hisia zangu kama Ifuatavyo ;
(I) BEN RABIU WA SAANANE AMETEKWA?; Hii ni moja kati ya hofu yangu kuu sana, hofu hii inachagizwa na namna ya mkingamo wa hali ya kisiasa katiia bara la Afrika kwa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wakosoaji wakubwa wa tawala za kiafrika, hutendwa vibaya sana na matabaka dola.., wanasiasa hawa ambao huonesha dhahiri rangi zao (kwa aina ya siasa ambayo huchagua kuitumia,) hukumbwa na madhara sana., ipo mifano mingi sana ya watu katika mataifa ya Afrika ambao walipotea, baadae ikaja kujulikana maiti zao zimetelekezwa au wao kupatikana wakiwa hai...,
Bara la Afrika ndilo lenye kuongoza kwa kupotea kwa wanaharakati, wanasiasa, waandishi wa habari na wakosoaji wenye mrengo na msimamo mkali dhidi ya vyama dola au serikali.., makundi hayo ndiyo yenye kuathirika sana.., watawala wengi hawapendi kuona ukosoaji dhidi yao, wafuasi wa watawala hao mara nyingi sana hutumia mamlaka zao kuwapa shuruba wakosoaji hao.., kuwateka, kuwatesa na Mara nyingine kuwaua kabisa (mifano mingi sana inapatikana katika nchi za bara hili la Afrika).., hofu ya kupotea kwa njia kuwekwa kwa ndugu yetu huyu ni kubwa sana!
katika dhahania hii kuna maswali kadhaa ya kujiuliza;
(a) nani amemteka Ben Rabiu Wa Saanane..,?
(b) kwanini Ben atekwe na watu hao wasiojulikana..,?
(c) kwani Ben ana hatarisha usalama wa nani hadi atekwe na watu wasiojulikana!?
(d) kama ametekwa kweli.. Kwanini watesi wake wasimuachie huru sasa au watelekeze maiti yake!?
.., majibu ya maswali hayo siwezi kuwa nayo hata kidogo.., lakini bado akili yangu na akili ya watu wengine inaweza kuendelea kuhoji na hata kuamini BEN ametekwa!
(II) BEN RABIU WA SAANANE, ANATEKELEZA SHUGHULI ZA CHAMA CHAKE; kuna akili nyingine katika dhahania zangu inaeleza wazi.., huyu mtu wetu atakuwa yuko salama salmini anatekeleza shughuli zake za chama.., kwa sababu gani...., chama chake (CHADEMA) kimewahi/hadi sasa ni mwajiri wa Ben Rabiu wa Saanane.., Ben amewahi kuhudumu pale Ufipa (makao makuu ya CDM) kama mkurugenzi wa idara ya utafiti, sera na mambo ya nje (kama sijakosea).., ingawa kuna taarifa zinakuja (zisizo rasmi sana) kwamba kitengo hicho kilifutwa katika teuzi mpya za wakurugenzi wa idara katika chama hicho.., hivyo BEN akabaki kuwa msaidizi binafsi (personal Secretary) wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Aikaeli Mbowe.., hadi hapo., luna maswali kadhaa naweza sasa kujiuliza mwenyewe hapa;
(a) kwanini Mbowe ambaye huyu (BEN) ni mtumishi wake binafsi (msaidizi binafsi), yupo kimya kuhusu suala hili hadi sasa..,!?
(b) kwanini CHADEMA, chama cha Ben (kama mwanachama) na mtumishi wa zamani wa chama hicho, hakioneshi 'aggressiveness' ya kutosha katika suala hili!?
(c) kwanini Chama na wanachama (baadhi) hawaoneshi kubeba suala hili kama ajenda yao mtambuka (hata kwa kufungua kesi ya kufukua miili ile 7 ileliyozikwa kule Bagamoyo) kutambua kama kuna BEN katika wale!?
(d) wabunge na wanachama wakubwa wale waamdamizi, hawaoneshi kabisa morali chanya ya kuandika katika mitandao, katika vyombo vya habari kuhusu kupotea kwa BEN.., kwa nini!?
Maswali hayo 4, mimi sina majibu nayo hata kidogo, na ndiyo maana namaliza kwa kuuliza.., na ndiyo maana nafika kwenye hitimisho la dhahania hiyo kwa kusema "labda..., BEN yupo salama, na viongozi wake, rafiki zake (baadhi) na hata ndugu zake wanatambua huyu mtu alipo"..,
Katika dhahania hii kuna ukiznzani.., ndugu wa BEN ndiyo walikuwa watu wa kwanza kabisa kuanza kupata hofu ya mahali alipo ndugu yao (wakatoa taarifa kwa marafiki wa BEN, na baadae polisi) hivyi inawezekana hawa hawatambui ndugu yao alipo.., swali la kujiuliza.., BEN yuko katika shughuli zake binfasi (labda) za masomo bila kujulisha ndugu zake!? Je, BEN yuko katika shughuli za chama bila kuwapa taarifa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu!? KWELI INAWEZEKANA!?
(III) BEN RABIU WA SAANANE, AMEAMUA KUJIWEKA MBALI NA MKONDO WA KISIASA; dhahania yangu ya mwisho kabisa ni kwamba; huyu msomi, mwanasiasa na kijana machachari mwenye weledi wa kutosha, ameamua kujiweka mbali na siasa.., kama ambavyo tunajua na kutambua..,
siasa za Afrika ni siasa zenye mapungufu mengi.., majungu, fitina, kebehi na kukatishana tamaa sana.., ni siasa zenye kupoteza muda wa wale ambao ni 'underdog' katika siasa.., ni aina ya siasa ambazo 'wale waliofanikiwa kisiasa hawapendi kuona wanasiasa wapya nyuma yao'...., pia ni aina ya siasa ambayo hutengeneza wafuasi na wapiga kura na siyo viongozi wa kesho..,
ni aina ya siasa ambayo imejaa watawala na siyo viongozi.., udikteta kwa hao watawala ni mkubwa na ukandamizaji kwa wale walio Chini ya watawala hao ni mkubwa..., labda sasa, BEN ameamua kujiweka mbali ma siasa kwa muda huu ili atimize malengo yake ya kupata shahada yake ya 3 (PhD).., ambayo yuko mbioni kuweza kuikamata..,
Lakini.., BEN hajaanza leo harakati za kisiasa, amesoma wakati wote akiwa katika harakati hizo.., ametumikia elimu yake kwa weledi mkubwa sana na wakati huo akitumikia na siasa kwa wakati mmoja.., sioni namna hoja hii ikipata nguvu, kwa sababu, ndugu, jamaa na rafiki zake wangelikuwa wanajua alipo hadi sasa (kama suala ni kuachana na siasa kwa sasa)..,
USHAURI WANGU ;
(i) CHADEMA, kama waajiri wa zamani wa Ben Rabiu wa Saanane, wanapaswa kutumia idara yao ya sheria kutafuta haki mahakamani ya kuomba kibali cha maiti zile ambazo ziliokotwa mto Ruvu na kuzikwa Bagamoyo (zifanyiwe uchunguzi wa kitabibu) kubaini sampuli za wale marehemu kwa kufananisha hata na ndugu zake na BEN.., (itasaidia kuachana na wazo hilo)
(ii) ifunguliwe kesi mahakamani, kupitia ndugu zake na BEN (Familia) na msaada wa taasisi ya kisiasa ambayo BEN amehudumu kama mtumishi wake, kuwalazamisha polisi na TCRA (mamlaka ya mawasiliano nchini) kufanya uchunguzi yakinifu wa wapi BEN ametumia simu yake kwa mara ya mwisho, amewasiliana na nani na watu gani amekuwa akiwasiliana mao mara kwa mara, (taarifa hizo zipo katika server ya mtandao wa simu aliokuwa anatumia BEN)
(iii) wanachama wenzake na BEN, marafiki zake.., wanapaswa kuanzisha vuguvugu hai la kumdai mwenzao (mwanachama mwenzao) kwa uongozi wa chama chao (hata kama haujui alipo) ili chama kitoe msaada anuwai wa kusema kwa sauti na kuchukua hatua anuwai za kudai na kushinikiza umma utambue upotevu wa mwenzao na hivyo vyombo vya dola, ulinzi ma usalama vitumie wakati na muda wao kwa nguvu sana kumtafuta mtanzania huyu..
(iv) bila kuchoka, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki wa BEN na wale wote ambao wanaguswa na tukio hili, waendelee na kampeni kubwa mitandaoni kwa kutumia hashtag maalum za kuonesha kumhitaji BEN.., zipo nyingi, mfano #BRINGBACKOURBEN #WENEEDOURBENBACK #BRINGBACKBRNALIVE #TUNAMTAKABENWETU na nyingine nyingi.. Hizi hashtag zinafikisha ujumbe kwenye jamii ya Dunia kwa haraka sana..,
(v) vyombo vya ulinzi na usalama (kupitia jeshi la polisi), lina- wajibu mkubwa sana wa kulinda usalama wa raia na mali zao, hivyo, wanapaswa kutoka hadharani, (hii habari ya kupotea kwa mtanzania kwa siku 32) ndani ya nchi yake, siyo habari ndogo, ni habari kubwa kweli-kweli.., inaweza kuchafua taswira ya taifa letu.., hivyo jeshi la polisi litoke nje hadharani na kueleza umma kuhusu mwenendo wa tukio hili (kuondoa hofu tanduzi katika vichwa vya marafiki, ndugu, jamaa wa Ben) Ben ni raia, hivyo jeshi la polisi lina wajibu wa kuwajibika kwa mtanzania huyu (mlipa kodi halali wa taifa hili)
MWISHO: i. Chama cha Demokrasia na maendeleo ambapo Ben amekuwa mwanachama na kiongozi, hatua ya kutoa tamko mara moja na kisha kukaa kimya haitoshi ikilinganishwa na umuhimu na na juhudi za Ben katika kukijenga chama hicho kama mwanachama na kiongozi / mfanyakazi katika makao makuu ya chama.
ii. Swala lililokaa kisiasa kama hili serikali kutokuchukua hatua kubwa zinazoonekana katika macho ya wananchi linatia mashaka hasa kwa wanaharakati ambao kupitia ukosoaji wao serikali inapata kujua maeneo ambayo inahitaji kufanyia marekebisho katika utendaji kiurahisi.