Saturday, 27 October 2018

Birthday Party (Isaya J Ngeleja)

Na Mwandishi wetu: Nascent Franzwa
Sat 27 Oct 2018 maeneo ya Artisan Kagera Sugar katika mkoa wa Kagera majira ya usiku unategemewa kuwa usiku Wa aina yake.

Hii ni kutokana na tukio la aina yake kuwahi kufanyika kama kumbukumbu ya birthday kutegemewa kufanyikia hapo.

Isaya Ngeleja (Graduate Trainee) kiwandani hapo anategemewa kufanya kumb. ya kuzaliwa kwa namna ambayo imeelezwa kuwa kufuru eneo hilo.
Usikose kufuatilia tukio hilo litakarushwa mubashara na Marambamedia

Saturday, 22 September 2018

AJALI MV NYERERE MAJONZI MWANZA

20 September 2018 majira ya Saa nane alasiri iligeuka simanzi jijini Mwanza na viunga vyake.
Hii ni baada ya kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Buhorora Ukerewe na Ukara (visiwani) kupata ajali kikiwa kinakaribia kabisa kutia nanga.Imeelezwa kuwa kivuko hicho huenda kilibeba uzito zaidi ya uwezo wake kwani hata idadi ya maiti zilizookolewa ni zaidi ya 131 huku walio hai wakiokolewa takribani 40 + Injinia mmoja aliyeokolewa baada ya siku mbili (Sept 22)
Kinachoshangaza ni kuwa vyombo vya usafiri majini huwa na mstari mweusi au mwekundu ambao haupaswi kuzama wote majini.Mstari kama ungeangaliwa kabla ya safari kuanza huenda ungesaidia kuona kama uzito umezidi au la hasha.Bado haijabainika kama ukaguzi huo ulifanyika.
Ni vema pia katika karne hii ya sayansi na technolojia kukawekwa madaraja ya kupimia uzito/Weight bridge/Mizani katika bandari zetu kama Bado hatujafanya hivyo ili kupunguza uwezekano wa ajali za uzembe kutokea kutokana na ukadiriaji wa kizamani.
Mungu azilaze roho za marehemu wetu mahali pema peponi.Amina

Sunday, 6 May 2018

Tanzia

May 6, 2018 ni siku moja kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha 6 nchini Tanzania, mwanafunzi mmoja ajiua kwa kujinyonga katika mti wa mwembe.

Mwanafunzi huyo Robert Masaba (21) ni mmoja wa wanafunzi waliohamishwa kutoka shule ya sekondari Nyakato manispaa ya Bukoba kwenda Kahororo baada ya shule ya Nyakato kuharibiwa na tetemeko lililokumba mkoa wa Kagera miaka 2 iliyopita, lililoanza mnamo 10 September 2016.

Aidha,mwanafunzi Robert(marehemu) mwenyeji wa wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliotegemewa kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha sita hapo kesho 2018 May 7.

Bado haijathibitika kwanini ameamua kufanya kitendo hicho kilicho kinyume na haki ya kuishi.
Mungu awasaidie waliobakia wafanye vema mitihani yao.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.

The Death of Death "Mwisho wa Kifo"

Kifo kitakuwa uamuzi kufikia mwaka 2045!!!!
Kufariki itakuwa 'chaguo' ndani tu ya miaka 27 na  mlolongo wa kuzeeka utakuwa 'unaogeuzika', kwa mujibu wa WAHANDISI JENITIKI WAWILI wakati wa uwasilisho wa kitabu chao kipya Barcelona.

José Luis Cordeiro, alizaliwa Venezuela na wazazi Wahispania, na Cambridge (UK) mwanamahesabu David Wood, mwanzilishi wa operating system 'Symbian', wamechapisha "The Death of Death" ie KIFO CHA KIFO au mwisho wa kifo kwa tafsiri isiyo rasmi, na kusema kutokufa ni sahihi na uwezekano wa kisayansi ambao ungekuja mapema zaidi zaidi ya ilivyofikiriwa awali.

Binadamu watafariki tu kwa ajali, kamwe si kwa asili ama ugonjwa, kufikia mwaka 2045, walisema Cordeiro na Wood, ambapo walisema ni 'muhimu' kwamba uzee unaanza kuainishwa kama  'ugonjwa' ili kwamba ufadhili wa umma katika tafiti juu ya 'tiba' yake uongezwe.

Nanoteknolojia ni ufunguo, kati ya mbinu nyingine mpya za uendeshaji vinasaba, Wahandisi walisema wakati wa uwasilisho wakiwa "Equestrian Circle "Barcelona.

Mchakato utahusisha ugeuzaji jeni 'mbaya' kuwa jeni bora, kuondoa seli zilizokufa mwilini, kukarabati seli zilizoharibiwa, matibabu kutumia seli za shina na 'kuchapisha' ogani muhimu katika 3D.

Cordeiro, ambaye yupo Massachusetts Institute of Technology (MIT) USA, alisema amechagua " Kutokufa" na kwamba katika kipindi cha miaka 30, atakuwa 'mdogo zaidi ya alivyo hivi sasa'.

Kuzeeka ni matokeo ya mikia ya DNA , iitwayo 'telomeres', katika kromosomu –ambapo kila seli isipokuwa seli nyekundu za damu seli jinsia, zina jozi 23 – zikifupika, na kukengeusha uzee  kunahusisha urefushaji wa telomeres.

Telomeres huharibika na kufupika kadiri muda usongavyo, mchakato uongezao kasi ya tukio la sumu kuingia mwilini– uvutaji, vileo na uchafuzi hewa ni kati ya mambo yanayoathiri urefu wa telomeres, hivyo kuchochea kuzeeka.

Cordeiro na Wood wanaamini kuwa  ndani ya miaka 10 , magonjwa kama  kansa yatakuwa yakitibika, na kwamba mashirika makubwa ya Kimataifa kama Google yataingia katika uwanja wa kitabibu "medicine" kwa sababu yanaanza kutambua kuwa "kutibu  kuzeeka inawezekana".

Microsoft tayari wameripoti kutengeneza kituo cha cryopreservation ambapo  Wanasayansi wanatafiti uwezekano wa kansa kutibika kabisa ndani ya muongo mmoja.

Wahandisi walielezea kuwa, ingawa 'watu kiujumla hawaelewei juu ya hilo', iligundulika mwaka 1951 ni namna gani seli kansa ni salama: wakati Henrietta Lacks alipofariki kwa kansa ya shingo ya kizazi "cervical cancer", upasuaji ulipoondoa tumor na kuihifadhi– na bado ipo  'hai' hivi sasa.

Kutokufa hakutamaanisha  sayari itazidiwa idadi ya watu, wanasayansi walisema: Bado kuna nafasi watu wengi duniani, na siku hizi, hakuna popote watu wenye watoto wengi kama ilivuokuwa kwa miongo na karne  zilizopita ; pia, 'itawezekana kuishi anga za mbali wakati huo'.

“Japan na Korea, kama wataendelea na tabia yao ya sasa ya kutokuzaa, watapotea kabisa – ndani ya karne 2, hakutakuwa na Mjapani au Mkorea duniani,” Alisema Cordeiro.

“Lakini asante kwa hii mbinu mpya, kweli wataendelea kuwepo Wajapani na Wakorea, kwa sababu wataishi milele na kubakia vijana.”

Gharama ya matibabu ya kuzuia uzee inalinganishwa na  ile ya  SimuJanja za karibuni.

“Mwanzoni, itakuwa ghali, lakini kwa soko shindani bei itapungua taratibu kwa sababu kitu kimnufaishacho kila mmoja,” Alisema Cordeiro.

“Teknolojia, ikiwa bado mpya, ni dhaifu na gharama sana, lakini hatimaye huwa ya kidemokrasia na kutawala na kuwa rahisi.”

Wahandisi wamesema kuwa tayari wamewekeza mbinu zao miaka 2 – kiharamu, lakini Colombia ambapo kuna taratibu chache zinazohusu uendeshaji genitiki.

Elisabeth Parrish, mgonjwa wao wa kwanza, 'alianza kuona dalili za kuzeeka na kuuliza kipi kingaliweza kufanyika ili kuzuuzuia'.

Matibabu yake ni 'hatari sana na haramu pia', Wood alieleza, lakini hivi sasa anaendelea vema, hayajatokea madhara yoyote yatokanayo na matibabu, na kiwango cha telomeres katika damu yake ni 'miaka 20 kiudogo zaidi ya kabla ya matibabu'.

“Nataka Hisapania iwe na  sehemu katika dunia ya hii mbinu na kuonesha kuwa sisi sio vichaa, ni vile watu bado hawawafahamu,” Wood alihitimisha.

Mwisho wa kifo "The Death of death" hatimaye kitachapishwa katika lugha nne kwa mara ta kwanza– Kihispania/Kihispaniola, Kingereza, Kireno na Kikorea – na mspato yote toka kwa mauzo yake yatawekezwa kwa  utafiti wa mwandishi.

 IMETAFSIRIWA NA Nascent Franzwa
nascentfrancium@yahoo.com
B.Sc Agriculture General
" Self-Proclaiming Extension Officer "

Saturday, 11 November 2017

Mh Rais Magufuli azuru KSL

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Joseph Pombe Magufuli alikuwa Rais wa kwanza kuzuru kiwanda cha kuzalisha sukari, ambapo Kagera Sugar imepata bahati hiyo katika kipindi cha takribani miaka 14 pasipo viwanda vya sukari kupata bahati hiyo.
Siku ya Jumatano tarehe 8 November 2017, siku mbili baada ya uzinduzi wa jengo la kisasa la abiria la uwanja wa ndege wa Bukoba.
Rais Magufuli ambaye amejipambanua kwa Sera ya Viwanda, amekuwa akihubiri Maendeleo ya uchumi wa kati ambayo amejizatiti kuyafikia kupitia uimarishaji wa Sera ya Viwanda ili Tanzania iweze kuneemeka moja kwa moja na rasilimali nyingi ilizo nazo.
Aidha, pamoja na kukimwagia kiwanda cha Kagera Sugar sifa nyingi, pia aliwaomba wamiliki wa viwanda vya sukari nchini Tanzania kumhakikishia kutokuwepo kwa upungufu wa sukari nchini,ambapo pia aliwapa nafasi ya kuchukua tenda ya uagizaji wa Sukari msimu usiokuwa wa uzalishaji Sukari nchini.Kwa kuwapatia vibali hivyo, Rais ana imani kuwa  ataweza kuzuia mianya ya uagizaji holela wa Sukari nje ya nchi ambayo inapelekea baadhi ya wafanyabiashara wasio waaminifu kuagiza Sukari isiyokuwa na ubora.

Aidha pia, Rais aliwaomba wazalishaji wote wa Sukari kuona ni namna gani wataweza kuongeza uzalishaji wa Sukari ili watakapofikia kiwango cha mahitaji kwa Taifa, aweze kuzuia kabisa uagizaji wa Sukari toka nje ya nchi.
Kiwango cha mahitaji ya sukari  kwa Mwaka ni takribani tani 450000 na upungufu takribani tani 130000.

Baada ya ziara hiyo Rais aliendelea na ziara yake ambapo alizuru taifa jirani la Uganda.

Friday, 3 March 2017

AJALI YA BASI YALETA MAJONZI SUA

Usiku wa Alhamisi ya tarehe 2 Feb 2017 uligeuka simanzi kwa Watanzania baada ya basi la abiri mali ya kampuni ya Ilyana kutokea Dar kwenda Songea kupata ajali maeneo ya Njombe .

Katika ajali hiyo watu watatu walipoteza maisha huku 28 wakijeruhiwa.Aidha, kati ya waliopoteza maisha, mmoja ni mwanamke na wawili ni wanaume.

Chanzo chetu cha habari kimeweza kupata jina la mmoja wa wanaume waliopoteza maisha kuwa ni Festo Nungu, ambaye alikuwa mwanafunzi wa mwaka wa mwisho katika Chuo kikuu cha Sokoine, katika Koleji ya Agriculture akiwa amebakisha semester moja kuhitimu shahada ya Kilimo mseto.

Mwenyezi Mungu azipumzishe roho za marehemu wote pema peponi.
Bwana alitwaa Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe.Amina

Sunday, 12 February 2017

BARUA YA WAZI KWA RAIS

BARUAKWENDA KWA RAIS JPM ILIYOANDIKWA NA ANSBERT NGURUMO

Mheshimiwa Rais John Magufuli, sijawahi kukuandikia barua, ama ya sanduku la posta au ya mtandaoni. Leo nakuandikia kupitia gazetini kwa sababu mbili:-

Kwanza, natambua kuwa wewe ni msomaji wa magazeti. Naulishanithibitishia kuwa hukosi kusoma maandishi yangu. Kwa hiyo najua utasoma.

Bahati nzuri, ninachokuandika si siri. Ni barua ya wazi itakayosomwa na Watanzania wengine. Lengo la kuiweka wazi ni kukuhamasisha nawe utambue kuwa mawasiliano ya kujenga nchi hayahitaji kufanyikia sirini au gizani.

Hii itakufanya uelewe kwanini wananchi hawachoki kuhoji sababu za serikali yako kufuta matangazo ya bunge ya moja kwa moja. Nakwambia bila kificho kuwa, hata mjieleze vipi, wananchi hawako tayari kuelewa kuwa katika karne hii, bunge lao linaondolewa kwenye nuru na kuingizwa kwenye giza.

Mwanzoni, wananchi, wakiongozwa na wabunge, walimkasirikia Nape Nnauye, waziri uliyempa dhamana ya habari, sanaa, utamaduni na michezo, wakidhani ndiye aliamuru TBC, Shirika la Utangazaji la Taifa, lisitishe matangazo ya moja kwa moja kwa kisingizio cha gharama; kwa sababu ndiye aliyetoa tangazo hilo bungeni.

Lakini sasa wanaelewa kuwa Nape hawezi kufanya uamuzi mkubwa kama huo bila kutumwa na mkubwa wake wa kazi. Na kwa jinsi wanavyokufahamu wewe, kama Nape angekuwa amefanya uamuzi huo wa kijinga bila kukuhusisha au bila kutumwa na wewe, ungekuwa ama umetengua uamuzi huo au umemtumbua jipu.

Kwa sababu hiyo, wananchi wameachanana Nape, wanakuandama wewe, na sasa wanasema jipu hilo ni lako. Unaogopa kujitumbua kwa kuwa mganga hajigangi. Ndiyo maana nimeamua nikutumbue.

Pili, mimi na Watanzania wamegundua kuwa katika masuala mengi ya kitaifa, unadanganywa. Vijana wa mjini wanasema unaingizwa mkenge. Na ukishadanganywa, nawe unaibuka na kudanganya wananchi.

Naomba utambue kuwa kwa kusema haya siombi kazi kwako. Ninayo. Na sehemu ya majukumu yangu kwa taifa hili ni kuuambia wewe ukweli mchungu bila woga au upendeleo.

Tabia yangu hii inasaidia kuziba mapengo ya wasaidizi wako ambao, licha ya kwamba wapo katika majengo wanayoita ofisi, kimsingi hawapo kazini, kwa kuwa hawafanyi kazi yao, hasa ya kukushauri viizuri.

Na baadhi yao wanasema kwamba hushauriki, unafanya utakalo, mara nyingi, bila kupima madhara ya uamuzi wako.

Wanasema hii ndiyo sababu inayokufanya utoe kauli tata au zinazopingana mara kadhaa.

Kwa mfano, mtu mmoja ameandika kwenye mtandao wa kijamii, akinukuu kauli yako uliyotoa kwa hasira mwezi Februari 2016 baada ya MCC, Shirika la Changamoto za Milenia, la Marekani, kukata misaada kwa Tanzania kwa sababu ya wizi wa kura Zanzibar na kutunga sheria katili ya makosa ya mtandaoni.

Siku ile, ulisema hivi: “Haiwezekani nchi tajiri kama Tanzania tuwe ombaomba. Sisi ndio tunatakwa kuombwa misaada.”

Kauli yako ilizua gumzo nchi nzima. Baadhi ya wananchi, wakiwemo marais wastaafu, walisema kuwa misaada kutoka nje haikwepeki, na kwamba hata kama kauli yako ina ukweli wa kimantiki, si kweli katika uhalisia kwa kuwa serikali yako, haijajipanga kujitegemea na kujitosheleza.

Wengine walikudhihaki kuwa umetoa kauli hiyo mithili ya simulizi la sungura aliyeruka akashindwa kufikia mkungu wa ndizi, hatimaye akasema kwa hasira, “sizitaki mbichi hizi!!”

Vibaraka wako, wakiwamo wasaidizi wako, walitetea hoja yako. Mungu si Athuman, juzi umetoa kauli nyingine ulipotembelewa na Balozi wa Mareakani nchini, akaahidi kuipatia serikali yako msaada mkubwa wa dola milioni 800.

Katika furaha uliyokuwa nayo, ulisema hivi mbele ya waandishi wa habari:

“Amekuja balozi kutuhakikishia kwamba watatoa hela kwa ajili ya Tanzania, na anasema sasa hivi watatoa zaidi ya dola milioni 800, na mkataba mwingine tunaweza kusaini hata kesho wa dola milioni 410….Fedha za msaada kutoka Marekani ni muhimu mno kwa maendeleo ya Tanzania.”

Tuna marais wangapi? Februari ulisema hutaki misaada; Juni unasema misaada ni muhimu. Tunapouliza wasaidizi wako kwanini wanakuacha unatoa kauli za ajabu ajabu, wanasema hupendi kushauriwa.

Wanasema kuwa wanaogopa kukuambia usichotaka kusikia, kwa sababu wameshakusoma, unapenda kusikiliza sauti yako mwenyewe na kutanguliza hisia zako, badala ya kufanyia kazi ushauri wa wataalamu.

Eti wakati mwingine wanakuandikia hotuba za kirais katika matukio muhimu, ukishafika eneo la tukio unagoma kuzisoma; unatoa maoni yako ya kichwani, ambayo wakati mwingine yanakufanya uonekane kama kamanda wa polisi bada ya rais wa nchi.

Wanasema, kwa mfano, siku ya maadhimisho wa Wiki ya Sheria, maneno uliyotoa mbele ya wanasheria waliobobea, huku ukimwagiza jaji mkuu, yalikuwa yamekataa tenge, na hayatekelezeki kisheria; ni amri zisizofanana na mfumo wa kidemokrasia na utendaji wa kisheria.

Hawakukuambia pale pale, lakini walikuteta baadaye. Kwanini unaruhusu mambo haya yatokee wakati una nyenzo za kuyazuia?

Mmoja ameniambia wiki hii kuwa kwa jinsi anavyoona unazungumza na unatenda, una nia nzuri na taifa hili, lakini unakosa mbinu za kiuongozi. Anasema unatenda kama meneja, si kiongozi.

Anasema vitu vingine unavyoagiza, au unavyoamua, unavifanya kama mtawala, si kama kiongozi. Na kwa kukosa tunu ya uongozi, utafanya mambo mengi mazuri juu juu lakini hayatadumu kwa sababu hayakujengwa juu ya msingi imara.

Utakuwa umefanikiwa kufanya mambo mema kwa muda mfupi, lakini yatafutika kirahisi kwa kuwa mtindo uliotumika kuyatekeleza si endelevu, bali zima moto.

Wasaidizi wako wanakuficha mambo ya msingi. Wanasema umezidi ukali, na huna subira wala simile, kiasi kwamba unaweza kumwaibisha mtu yeyote mahali popote, bila kujali cheo au hadhi yake.

Na unawafanyia wenzako hivyo, lakini wewe hutaki kuguswa au kusahihishwa. Unalinda cheo chako, unadhalilisha vyeo vyao.

Kama ulikuwa hujajua, washauri wako sasa wana msimamo rasmi, kwamba watakushauri kwa kuzingatia kile unachotaka kusikia kutoka kwao.

Kama msimamo huu utadumu, mheshimiwa rais utaangamiza nchi. Kama unafurahia kuongoza nchi ya watu waoga, ujue nchi hiyo si Tanzania tunayotaka kujenga, au ile unayozungumzia kwenye hotuba zako.

Mazuri yote unayohubiri kwenye hotuba zako, yatatumika kukukejeli baada ya muda wako wa kukaa Ikulu kuisha.

Wanakutii, lakini hawakupendi. Na kwa sababu unawapuuza, wakipata fursa watakuhujumu.

Hata hivyo, wapo pia wanaodhani kwamba huna washauri wazuri. Mtu mmoja amesema; “Tatizo ninaloona sasa hivi, wasaidizi wa rais wanashindwa kutafsiri dira na ajenda yake. Hawamwelewi, naye haeleweki kwao.

“Apende asipende, anahitaji semina elekezi. Uamuzi unaochukuliwa na wasaidizi wake unatokana na tafsiri yao ya dira yake. Wengi wanafanya kwa woga na kulinda ajira zao tu.

“Panapohitajika ushauri wa kitaalamu wanapatwa na ugonjwa wa kupooza, kwa sababu wanaangalia matokeo ya kisiasa na uhusiano wao na rais. Tuanze kujiuliza, rais anaposema ‘Hapa Kazi Tu, ana maana gani?”

Huyu alisema hivi baada ya jeshi la polisi kuzuia mikutano ya wanasiasa kwa sababu zile zile za miaka nenda rudi. Hawakui. Hawaelimiki. Na baadhi ya wakuu katika jeshi la polisi wanadai kuwa “wamefanya hivyo kwa kufuata “maagizo kutoka juu.” Huko juu ni wapi kama si Ikulu?

Uamuzi huu wa kuzuia mikutano ya vyama vya siasa, kwa hofu kwamba itawafanya wananchi waelewe udhaifu wa serikali ya awamu ya tano, na kukuza upinzani ambao umesema mara kadhaa kwamba una nia ya kuuua, unakutia doa.

Uamuzi huu unakuondolea taswira ya ujasiri unayojijengea majukwaani unapokuwa unafoka. Sasa wananchi wanahoji: “Kumbe anafoka kuficha udhaifu wake!”

Ushauri, wangu kwako ni huu: Ongoza nchi, usiitawale. Acha wananchi wapumue. Zungumza nao, usiwahutubie. Sikiliza washauri wasiojikomba kwako.

Kumbuka kuwa nchi hii si ya rais na baraza la mawaziri, bali ni ya wananchi uliokuwa unawaomba kura na kuwaburudisha kwa maneno matamu na pushapu jukwaani. Hawa ndio waajiri wako. Wasikilize. Jifunze kwamba ubabe hautawali nchi yotote katika karne ya sasa.

Wananchi wanatazama mbele, hawatakubali kurudishwa nyuma, hata kwa mabavu

Friday, 10 February 2017

UTALII WA NDANI

Feb 10 2017 nilipata bahati ya kutembelea hifadhi ya Taifa ya wanyama nchini Tanzania ijulikanayo kama Mikumi.

Mikumi ni hifadhi ya 4 kwa ukubwa ikitanguliwa na Serengeti, Ngorongoro na Manyara.

Hifadhi hii ipo katika mkoa wa Morogoro kati ya barabara iendayo Iringa.Ni hifadhi iliyosheheni wanyama wengi wa porini ikiwemo jamii ya swala,nyati,nyumbu, pundamilia, tembo, twiga, Simba na Chui.

Kilichonivutia zaidi ni juu ya Twiga.Huyu ni mnyama mwenye uwezo mkubwa wa kutofautisha rangi mbalimbali ikilinganishwa na wanyama wengine.Wao huweza tu kutofautisha nyeupe na nyeusi.

Mnyama huyo anapoona kitu kigeni hutulia mithili ya sanamu kwa ajili ya kuweza kukitambua na kama ni adui aweze kujua namna ya kujihami.

Kinachovutia zaidi ni mwondoko wake hasa anapotembea mwendo wa pole. Kutokana na muundo wa shingo yake pamoja na miguu yake, atembeapo mnyumbuliko Wa mwili wake huvutia mithili ya mwanadada mrembo awapo katika kupita mbele ya majaji ili apate kura za unenguaji.

Pamoja na hayo yote, Moyo Wa twiga huweza kukua hadi kufikia kilo 12 na hivyo hii humfanya kushindwa kuwa na mzunguko mzuri wa damu endapo atalala. Ili kuepusha shida, alalapo hukunja miguu na kulalia kifua, huku shingo ikiwa juu ama kuegeshwa kwenye mti.

Sunday, 29 January 2017

SAT212017

Ni Jumamosi ya tatu ya mwaka 2017 ambapo ilishihudiwa sherehe kubwa ya kumpongeza Shemasi Alfredi Fadhili Frimin huko kijijini kwao Kooti katika Kata ya Olele tarafa ya Mashati Wilayani Rombo Kilimanjaro.

Friday, 23 December 2016

Heri ya Krismasi na Mwakampya 2017

Anaandika *Nascent Franzwa*
Jmos Dec 24 2016

*Christmass ikufanye mtu bora*

Tarehe 25 kila Dec ni siku ambayo Wa Kristo walio wengi huitumia siku hiyo wakikumbuka ujio wa Masiha kwa mara ya kwanza duniani kupitia kwa Bikira aitwaye Marimu, zaidi ya miaka 2000 iliyopita.

Watu wengi huitumia siku hii kwa namna mbali mbali ikiwepo kufurahia na familia zao, kutembelea maeneo mbali mbali na kwa kusali.

Mara kadhaa katika sikukuu kubwa kama hii vimekuwepo visa kadhaa ambavyo vimekuwa vikisababisha maafa mathalani kuwaachia watoto kwenda katika kumbi za starehe za watoto ambazo hazina ubora na ulinzi wa kutosha.

Kama wazazi tunajukumu la kuhakikisha kuwa tutaacha vitabia hivyo na kuwa watu wapya kwa kuwa karibu zaidi na watoto wetu hasa wadogo ili kuepusha changamoto za maafa kwa watoto kujirudia.

Uongozi wa Marambamedia unawatakia watu wote sherehe njema za Kuzaliwa Kristo pamoja na Mwakampya wenye heri na fanaka.

Tuoneshe upendo kwa wote

©Marambamedia2016

Tuesday, 20 December 2016

MichezoniLeo2016Dec21

CAMEROON GIZA NENE
Jan 14 2018 kivumbi cha Afcon kitaanza kutimka kule Gambia. Hata hivyo, wakati mataifa shiriki yakiwa katika maandalizi, Cameroon huenda ikawakosa nyota wake saba kutokana na kile kocha wake Hugo Broos amekieleza kuwa ni maslahi binafsi ya nyota hao.

Nyota hao ni Beki mahiri wa Liverpool Joe Matip, Allan Nyom wa West Bromwich, Andre Onana wa Ajax Amsterdam, Guy N'dy Assembe wa Nancy, Maxime Poundje wa Girondins Bordeaux, Andre-Frank Zambo Anguisa wa Olimpique Marseille pamoja na Ibrahim Amadou wa Lille
(Chanzo: BBC)

REAL MADRID YAPATA AHUENI
Real Madrid imepunguziwa adhabu iliyotolewa na Fifa kutokana na kosa la kukiuka kanuni za usajili wa wachezaji wa umri wa chini ya miaka 18

Mahakama ya usuluhishi wa michezo(CAS) imewapunguzia adhabu hiyo kutoka kutosajili hadi Jan 2018 na badala yake kuanza usajili baada ya July 2017. Pia faini waliyotozwa na Fifa kwa kosa hilo imepunguzwa kutoka pauni 282,000 hadi Pauni 188,000.

VARY KUKOSA MECHI TATU
Mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy atalazimika kukaa nje ya Dimba hadi Jan 7 2018 ambapo atarejea wakati wa mchezo wao dhidi ya Everton kombe la FA mzunguko wa 3.
Hii ni baada ya rufaa ya timu yake kutupiliwa mbali na FA. Vardy alipewa kadi nyekundu alipomchezea vibaya Mame Diouf.
Michezo atakayoikosa Vardy ni ule wa Everton utakaochezewa ugenini katika dimba la Goodson Park, wa West Ham pale King Power na wa Middles brough Jan 02 018.

VPL MWISHO WA WIKI
Ijumaa hii 23Dec utakuwepo mtanange wa African Lyon vs Yanga watakaomenyana pale Shamba la Bibi saa kumi na nusu jioni.

Jumamosi 24Dec;
Majimaji vs Azam Fc uwanja wa Majimaji saa kumi kamili jioni.

Mwadui Fc vs Mbao Fc uwanja wa Mwadui Complex saa kumi kamili jioni.

Simba Sc vs JKT Ruvu Shamba la Bibi saa kumi kamili jioni.

©marambamedia.blogspot.com2016

Habari Kuu 20 Dec

Trump aidhinishwa rasmi kuwa Rais wa 45 wa Marekani.

Siku 32 za kupotea kwa Mwanaharakati wa Chama Kikuu cha upinzani nchini Tanzania , CHADEMA ,Ndg Ben Saanane bado ni fumbo zito.

Balozi wa Urusi nchini Uturuki Bwana Andrey Karlov auawa kwa kupigwa risasi akiwa katika ufunguzi wa maonesho ya sanaa. Rais Vladimir Putin amekitaja kitendo hicho kama uchokozi.

Mkurugenzi mtendaji wa mtandao maarufu Afrika Mashariki na Kati Jamii Forum Ndugu Maxence Melo aachiwa huru kwa dhamana huko nchini Tanzania.

Nchini DRC milio ya risasi imesikika maeneo kadhaa ya miji ikiwemo miji nikiwa ya Kinshasa na Lubumbashi kutokana na kutokuelewana kati ya upinzani na serikali juu ya muda wa nyongeza wa Joseph Kabila kusalia madarakani baada ya muhula wake kuisha usiku wa kuamkia Leo 20 Dec 2016.

Ripoti za shirika la Afya duniani zimeeleza kuwa, idadi inayokadiriwa kuwa sawa na nusu ya watu wazima barani Afrika wanakabiliwa na tatizo la Shinikizo la damu (Pressure) na hivyo kuifanya Afrika kuwa na kiwango cha juu cha tatizo hilo duniani kwa mujibu wa WHO.

Katika Michezo: Mwanadada Evelyene Njambi Thungu kutoka Kenya ameingia katika orodha ya warembo watano bora katika shindano la Malkia wa urembo duniani 2016 lililofanyika huko Marekani. Kwa sasa ndiye Malkia wa urembo barani Afrika.

SAKATA LA BEN SAANANE

Ikiwa zimepita siku 32 tangu kupotea katika katika namna isiyoeleweka kwa Mwanaharakati Ben Rabiu Wa Saanane mnamo Nov 18, 2016, hizi ni baadhi ya dhahania zilizopo katika mawazo ya Watanzania wengi.

Suala hili naligawanya katika matabaka 3 (yenye kujengwa na dhahania siyo uhalisia)., na matabaka hayo yote yana nguvu kubwa ya hisia hasi au chanya kuhusu sakata hili la ndugu yetu huyu.., nitafafanua matabaka ya fikra na hisia zangu kama Ifuatavyo ;

(I) BEN RABIU WA SAANANE AMETEKWA?; Hii ni moja kati ya hofu yangu kuu sana, hofu hii inachagizwa na namna ya mkingamo wa hali ya kisiasa katiia bara la Afrika kwa wanasiasa wa upinzani, wanaharakati na wakosoaji wakubwa wa tawala za kiafrika, hutendwa vibaya sana na matabaka dola.., wanasiasa hawa ambao huonesha dhahiri rangi zao (kwa aina ya siasa ambayo huchagua kuitumia,) hukumbwa na madhara sana., ipo mifano mingi sana ya watu katika mataifa ya Afrika ambao walipotea, baadae ikaja kujulikana maiti zao zimetelekezwa au wao kupatikana wakiwa hai...,

Bara la Afrika ndilo lenye kuongoza kwa kupotea kwa wanaharakati, wanasiasa, waandishi wa habari na wakosoaji wenye mrengo na msimamo mkali dhidi ya vyama dola au serikali.., makundi hayo ndiyo yenye kuathirika sana.., watawala wengi hawapendi kuona ukosoaji dhidi yao, wafuasi wa watawala hao mara nyingi sana hutumia mamlaka zao kuwapa shuruba wakosoaji hao.., kuwateka, kuwatesa na Mara nyingine kuwaua kabisa (mifano mingi sana inapatikana katika nchi za bara hili la Afrika).., hofu ya kupotea kwa njia kuwekwa kwa ndugu yetu huyu ni kubwa sana!

katika dhahania hii kuna maswali kadhaa ya kujiuliza;

(a) nani amemteka Ben Rabiu Wa Saanane..,?
(b) kwanini Ben atekwe na watu hao wasiojulikana..,?
(c) kwani Ben ana hatarisha usalama wa nani hadi atekwe na watu wasiojulikana!?
(d) kama ametekwa kweli..  Kwanini watesi wake wasimuachie huru sasa au watelekeze maiti yake!?

.., majibu ya maswali hayo siwezi kuwa nayo hata kidogo.., lakini bado akili yangu na akili ya watu wengine inaweza kuendelea kuhoji na hata kuamini BEN ametekwa!

(II) BEN RABIU WA SAANANE, ANATEKELEZA SHUGHULI ZA CHAMA CHAKE; kuna akili nyingine katika dhahania zangu inaeleza wazi.., huyu mtu wetu atakuwa yuko salama salmini anatekeleza shughuli zake za chama.., kwa sababu gani...., chama chake (CHADEMA) kimewahi/hadi sasa ni mwajiri wa Ben Rabiu wa Saanane.., Ben amewahi kuhudumu pale Ufipa (makao makuu ya CDM) kama mkurugenzi wa idara ya utafiti, sera na mambo ya nje (kama sijakosea).., ingawa kuna taarifa zinakuja (zisizo rasmi sana) kwamba kitengo hicho kilifutwa katika teuzi mpya za wakurugenzi wa idara katika chama hicho.., hivyo BEN akabaki kuwa msaidizi binafsi (personal Secretary) wa mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Aikaeli Mbowe.., hadi hapo., luna maswali kadhaa naweza sasa kujiuliza mwenyewe hapa;

(a) kwanini Mbowe ambaye huyu (BEN) ni mtumishi wake binafsi (msaidizi binafsi), yupo kimya kuhusu suala hili hadi sasa..,!?
(b) kwanini CHADEMA, chama cha Ben (kama mwanachama) na mtumishi wa zamani wa chama hicho, hakioneshi 'aggressiveness' ya kutosha katika suala hili!?
(c) kwanini Chama na wanachama (baadhi) hawaoneshi kubeba suala hili kama ajenda yao mtambuka (hata kwa kufungua kesi ya kufukua miili ile 7 ileliyozikwa kule Bagamoyo) kutambua kama kuna BEN katika wale!?
(d) wabunge na wanachama wakubwa wale waamdamizi, hawaoneshi kabisa morali chanya ya kuandika katika mitandao, katika vyombo vya habari kuhusu kupotea kwa BEN.., kwa nini!?

Maswali hayo 4, mimi sina majibu nayo hata kidogo, na ndiyo maana namaliza kwa kuuliza.., na ndiyo maana nafika kwenye hitimisho la dhahania hiyo kwa kusema "labda..., BEN yupo salama, na viongozi wake, rafiki zake (baadhi) na hata ndugu zake wanatambua huyu mtu alipo"..,

Katika dhahania hii kuna ukiznzani.., ndugu wa BEN ndiyo walikuwa watu wa kwanza kabisa kuanza kupata hofu ya mahali alipo ndugu yao (wakatoa taarifa kwa marafiki wa BEN, na baadae polisi) hivyi inawezekana hawa hawatambui ndugu yao alipo.., swali la kujiuliza.., BEN yuko katika shughuli zake binfasi (labda) za masomo bila kujulisha ndugu zake!? Je, BEN yuko katika shughuli za chama bila kuwapa taarifa ndugu, jamaa na marafiki zake wa karibu!? KWELI INAWEZEKANA!?

(III) BEN RABIU WA SAANANE, AMEAMUA KUJIWEKA MBALI NA MKONDO WA KISIASA; dhahania yangu ya mwisho kabisa ni kwamba; huyu msomi, mwanasiasa na kijana machachari mwenye weledi wa kutosha, ameamua kujiweka mbali na siasa.., kama ambavyo tunajua na kutambua..,

siasa za Afrika ni siasa zenye mapungufu mengi.., majungu, fitina, kebehi na kukatishana tamaa sana.., ni siasa zenye kupoteza muda wa wale ambao ni 'underdog' katika siasa.., ni aina ya siasa ambazo 'wale waliofanikiwa kisiasa hawapendi kuona wanasiasa wapya nyuma yao'...., pia ni aina ya siasa ambayo hutengeneza wafuasi na wapiga kura na siyo viongozi wa kesho..,

ni aina ya siasa ambayo imejaa watawala na siyo viongozi.., udikteta kwa hao watawala ni mkubwa na ukandamizaji kwa wale walio Chini ya watawala hao ni mkubwa..., labda sasa, BEN ameamua kujiweka mbali ma siasa kwa muda huu ili atimize malengo yake ya kupata shahada yake ya 3 (PhD).., ambayo yuko mbioni kuweza kuikamata..,

Lakini.., BEN hajaanza leo harakati za kisiasa, amesoma wakati wote akiwa katika harakati hizo.., ametumikia elimu yake kwa weledi mkubwa sana na wakati huo akitumikia na siasa kwa wakati mmoja.., sioni namna hoja hii ikipata nguvu, kwa sababu, ndugu, jamaa na rafiki zake wangelikuwa wanajua alipo hadi sasa (kama suala ni kuachana na siasa kwa sasa)..,

USHAURI WANGU ;

(i) CHADEMA, kama waajiri wa zamani wa Ben Rabiu wa Saanane, wanapaswa kutumia idara yao ya sheria kutafuta haki mahakamani ya kuomba kibali cha maiti zile ambazo ziliokotwa mto Ruvu na kuzikwa Bagamoyo (zifanyiwe uchunguzi wa kitabibu) kubaini sampuli za wale marehemu kwa kufananisha hata na ndugu zake na BEN.., (itasaidia kuachana na wazo hilo)

(ii) ifunguliwe kesi mahakamani, kupitia ndugu zake na BEN (Familia) na msaada wa taasisi ya kisiasa ambayo BEN amehudumu kama mtumishi wake, kuwalazamisha polisi na TCRA (mamlaka ya mawasiliano nchini) kufanya uchunguzi yakinifu wa wapi BEN ametumia simu yake kwa mara ya mwisho, amewasiliana na nani na watu gani amekuwa akiwasiliana mao mara kwa mara, (taarifa hizo zipo katika server ya mtandao wa simu aliokuwa anatumia BEN)

(iii) wanachama wenzake na BEN, marafiki zake.., wanapaswa kuanzisha vuguvugu hai la kumdai mwenzao (mwanachama mwenzao) kwa uongozi wa chama chao (hata kama haujui alipo) ili chama kitoe msaada anuwai wa kusema kwa sauti na kuchukua hatua anuwai za kudai na kushinikiza umma utambue upotevu wa mwenzao na hivyo vyombo vya dola, ulinzi ma usalama vitumie wakati na muda wao kwa nguvu sana kumtafuta mtanzania huyu..

(iv) bila kuchoka, wananchi, ndugu, jamaa na marafiki wa BEN na wale wote ambao wanaguswa na tukio hili, waendelee na kampeni kubwa mitandaoni kwa kutumia hashtag maalum za kuonesha kumhitaji BEN.., zipo nyingi, mfano  #BRINGBACKOURBEN  #WENEEDOURBENBACK #BRINGBACKBRNALIVE #TUNAMTAKABENWETU na nyingine nyingi..  Hizi hashtag zinafikisha ujumbe kwenye jamii ya Dunia kwa haraka sana..,

(v) vyombo vya ulinzi na usalama (kupitia jeshi la polisi), lina- wajibu mkubwa sana wa kulinda usalama wa raia na mali zao, hivyo, wanapaswa kutoka hadharani, (hii habari ya kupotea kwa mtanzania kwa siku 32) ndani ya nchi yake, siyo habari ndogo, ni habari kubwa kweli-kweli.., inaweza kuchafua taswira ya taifa letu.., hivyo jeshi la polisi litoke nje hadharani na kueleza umma kuhusu mwenendo wa tukio hili (kuondoa hofu tanduzi katika vichwa vya marafiki, ndugu, jamaa wa Ben) Ben ni raia, hivyo jeshi la polisi lina wajibu wa kuwajibika kwa mtanzania huyu (mlipa kodi halali wa taifa hili)

MWISHO: i. Chama cha Demokrasia na maendeleo ambapo Ben amekuwa mwanachama na kiongozi, hatua ya kutoa tamko mara moja na kisha kukaa kimya haitoshi ikilinganishwa na umuhimu na na juhudi za Ben katika kukijenga chama hicho kama mwanachama na kiongozi / mfanyakazi katika makao makuu ya chama.

ii. Swala lililokaa kisiasa kama hili serikali kutokuchukua hatua kubwa zinazoonekana katika macho ya wananchi linatia mashaka hasa kwa wanaharakati ambao kupitia ukosoaji wao serikali inapata kujua maeneo ambayo inahitaji kufanyia marekebisho katika utendaji kiurahisi.

Saturday, 16 July 2016

TCU YATOA MAELEZO YA MAREKEBISHO KUHUSU SIFA ZA KUDAHILIWA KUSOMA SHAHADA MWAKA HUU

















 

Tume ya vyuo vikuu nchini Tanzania imejitokeza leo tarehe 16  July 2016 na kutolea maelezo kuhusu utata ulikuwepo kuhusu wakina nani wana sifa ya kusoma degree kwa mwaka wa masomo 2016/17.....
Kwa mujibu wa tangazo lilotolew kwa umma na Katibu mtendaji wa TCU hivi leo ni kuwa tofauti na ilivyoeleweka mara baada ya marekebisho ya vigezo vya kusoma shahada hapa nchini, kwamba ni lazima kupata D mbili ili udahiliwe sio sahihi.....

Kwa mujibu wa tangazo hilo, inatakiwa mhitimu wa kidato cha sita awe najumla ya point 4 katika masomo mawili kati ya matatu ya mchepuo aliosoma......Hivyo mtu aliye na Ufaulu wa C na E atasoma shahada....
Mchanganuo kwa mwaka 2013 kurudi nyuma na mwaka 2016 , A=5, B=4, C=3, D=2, E= 1
Kwa wahitimu wa mwaka 2014-2015, matokeo yao yalukuwa katika mfumo tofauti..Kwao A=A=5, B+=B=4, B=C=3, C=D=2, D=E=1..............Kwa sababu hii, ilivyohesabika awali kuwa ni lazima kuwa na D mbili ndio udahiliwe sio sahihi.....Kwa maelezo zaidi tembelea kiungo cha tovuti ya TCU hapa chini.
 www.tcu.go.tz

Tuesday, 12 July 2016

IFAHAMU WILAYA YA ROMBO

best coffee beans
Mti wa buni





Mgomba

https://upload.wikimedia.org/wikipedia/en/2/2b/Map_of_Kilimanjaro_Region_%28Rombo_District_highlighted%29.gif
Ramani ya Mkoa wa Kilimanjaro
Rombo ni moja kati ya wilaya 7 zinazounda mkoa wa Kilimanjaro. Imegawanyika katika tarafa 5 zenye jumla ya kata 24. Tarafa hizo ni Tarakea, Usseri, Mashati, Mkuu pamoja na Mengwe. Hapa chini ni majina ya Kata zote za Rombo (W)
  • Aleni
  • Holili
  • Katangara Mrere
  • Kelamfua Mokala
  • Keni Mengeni
  • Kirongo Samanga
  • Kirwa Keni
  • Kisale Msaranga
  • Kitirima Kingachi
  • Mahida
  • Makiidi
  • Mamsera
  • Manda
  • Marangu Kitowo
  • Mengwe
  • Motamburu Kitendeni
  • Mrao Keryo
  • Nanjara Reha
  • Ngoyoni
  • Olele
  • Shimbi
  • Tarakea Motamburu
  • Ubetu Kahe
  • Ushiri Ikuini
Wilaya nyingine za mkoa wa Kilimanjaro ni
Mipaka
·         Upande wa Kaskazini na Mashariki Rombo imepakana na Nchi ya Kenya
·         Upande wa Magharibi wilaya ya Rombo imepakana na wilaya za Siha na Hai
·         Upande wa Kusini wilaya ya Rombo imepakana na wilaya ya Moshi vijijini
Idadi ya watu: Rombo inakadiriwa kuwa na idadi ya watu takribani 260,963 kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012.
Mazao makuu: Rombo ni kati ya wilaya maarufu nchini Tanzania kwa kilimo cha zao la Ndizi na Buni aina ya arabika.
Utamaduni: Rombo kama ilivyo kwa wilaya nyingine za Mkuoa wa Kilimanjaro, ni kati ya wilaya ambazo mwamko wa kielimu upo juu tangu zamani. Hata hivyo siku za karibuni ulevi wa pombe za kienyeji umeshamiri sana hali ambayo inchangia kupungua kwa uzalishaji katika kilimo na hata wakati mwingine baadhi ya watoto kulazimika kukatisha masomo kutokana na hali duni ya kimaisha. Baadhi ya majina ya pombe hizo ni pamoja na Mbege, Dadii, Busa, Kimorali, Kamchape, Ngongo, Banana, Chibuku pamoja na pombe zilizorasimishwa.
Vyakula vya kiasili katika wilaya ya Rombo ni vile vinavyotokana na ndizi kwa mfano Machalari, Kiburu, Kena, Mtori, Ng’ande, Irembwe hutengenezwa kwa kutumia mbaazi,maharagwe au kunde, pamoja na Ngararimo ambazo hutengenezwa kwa kutumia mahindi…….
Nini Kisichofahamika kuhusu Rombo ???????????
Kama nilivyoeleza hapo juu, hali ya Unywaji wa pombe kwa rika zote umekuwa ukiongeaeka katika karne hii ya 21 hususani kwa kati ya miaka 10 iliyopita kwa sababu mbalimbali zikiwepo msongo wa mawazo, udadisi pamoja msukumo wa marafiki (Peer presure)

1. JE, UNADHANI NINI KIFANYIKE ILI KUKINUSURU KIZAZI CHA SASA DHIDI YA MATUMIZI MAKUBWA YA POMBE ?????????

2. JE, TATIZO HILI LAWEZA KUISHA???????

3. JE, NANI ALAUMIWE KUTOKANA NA TATIZO HILI??????

4. JE, NINI MAONI YAKO DHIDI YA MATUMIZI YA POMBE??????

5. JE, POMBE INA MADHARA GANI KATIKA UKUAJI WA UCHUMI WA TAIFA NA JAMII ILIYOSTAARABIKA???????