Sunday, 6 May 2018

Tanzia

May 6, 2018 ni siku moja kabla ya kuanza kwa mitihani ya kidato cha 6 nchini Tanzania, mwanafunzi mmoja ajiua kwa kujinyonga katika mti wa mwembe.

Mwanafunzi huyo Robert Masaba (21) ni mmoja wa wanafunzi waliohamishwa kutoka shule ya sekondari Nyakato manispaa ya Bukoba kwenda Kahororo baada ya shule ya Nyakato kuharibiwa na tetemeko lililokumba mkoa wa Kagera miaka 2 iliyopita, lililoanza mnamo 10 September 2016.

Aidha,mwanafunzi Robert(marehemu) mwenyeji wa wilaya ya Kwimba mkoa wa Mwanza alikuwa miongoni mwa wanafunzi waliotegemewa kuanza mitihani yao ya kuhitimu kidato cha sita hapo kesho 2018 May 7.

Bado haijathibitika kwanini ameamua kufanya kitendo hicho kilicho kinyume na haki ya kuishi.
Mungu awasaidie waliobakia wafanye vema mitihani yao.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa; jina la Bwana na libarikiwe.

The Death of Death "Mwisho wa Kifo"

Kifo kitakuwa uamuzi kufikia mwaka 2045!!!!
Kufariki itakuwa 'chaguo' ndani tu ya miaka 27 na  mlolongo wa kuzeeka utakuwa 'unaogeuzika', kwa mujibu wa WAHANDISI JENITIKI WAWILI wakati wa uwasilisho wa kitabu chao kipya Barcelona.

José Luis Cordeiro, alizaliwa Venezuela na wazazi Wahispania, na Cambridge (UK) mwanamahesabu David Wood, mwanzilishi wa operating system 'Symbian', wamechapisha "The Death of Death" ie KIFO CHA KIFO au mwisho wa kifo kwa tafsiri isiyo rasmi, na kusema kutokufa ni sahihi na uwezekano wa kisayansi ambao ungekuja mapema zaidi zaidi ya ilivyofikiriwa awali.

Binadamu watafariki tu kwa ajali, kamwe si kwa asili ama ugonjwa, kufikia mwaka 2045, walisema Cordeiro na Wood, ambapo walisema ni 'muhimu' kwamba uzee unaanza kuainishwa kama  'ugonjwa' ili kwamba ufadhili wa umma katika tafiti juu ya 'tiba' yake uongezwe.

Nanoteknolojia ni ufunguo, kati ya mbinu nyingine mpya za uendeshaji vinasaba, Wahandisi walisema wakati wa uwasilisho wakiwa "Equestrian Circle "Barcelona.

Mchakato utahusisha ugeuzaji jeni 'mbaya' kuwa jeni bora, kuondoa seli zilizokufa mwilini, kukarabati seli zilizoharibiwa, matibabu kutumia seli za shina na 'kuchapisha' ogani muhimu katika 3D.

Cordeiro, ambaye yupo Massachusetts Institute of Technology (MIT) USA, alisema amechagua " Kutokufa" na kwamba katika kipindi cha miaka 30, atakuwa 'mdogo zaidi ya alivyo hivi sasa'.

Kuzeeka ni matokeo ya mikia ya DNA , iitwayo 'telomeres', katika kromosomu –ambapo kila seli isipokuwa seli nyekundu za damu seli jinsia, zina jozi 23 – zikifupika, na kukengeusha uzee  kunahusisha urefushaji wa telomeres.

Telomeres huharibika na kufupika kadiri muda usongavyo, mchakato uongezao kasi ya tukio la sumu kuingia mwilini– uvutaji, vileo na uchafuzi hewa ni kati ya mambo yanayoathiri urefu wa telomeres, hivyo kuchochea kuzeeka.

Cordeiro na Wood wanaamini kuwa  ndani ya miaka 10 , magonjwa kama  kansa yatakuwa yakitibika, na kwamba mashirika makubwa ya Kimataifa kama Google yataingia katika uwanja wa kitabibu "medicine" kwa sababu yanaanza kutambua kuwa "kutibu  kuzeeka inawezekana".

Microsoft tayari wameripoti kutengeneza kituo cha cryopreservation ambapo  Wanasayansi wanatafiti uwezekano wa kansa kutibika kabisa ndani ya muongo mmoja.

Wahandisi walielezea kuwa, ingawa 'watu kiujumla hawaelewei juu ya hilo', iligundulika mwaka 1951 ni namna gani seli kansa ni salama: wakati Henrietta Lacks alipofariki kwa kansa ya shingo ya kizazi "cervical cancer", upasuaji ulipoondoa tumor na kuihifadhi– na bado ipo  'hai' hivi sasa.

Kutokufa hakutamaanisha  sayari itazidiwa idadi ya watu, wanasayansi walisema: Bado kuna nafasi watu wengi duniani, na siku hizi, hakuna popote watu wenye watoto wengi kama ilivuokuwa kwa miongo na karne  zilizopita ; pia, 'itawezekana kuishi anga za mbali wakati huo'.

“Japan na Korea, kama wataendelea na tabia yao ya sasa ya kutokuzaa, watapotea kabisa – ndani ya karne 2, hakutakuwa na Mjapani au Mkorea duniani,” Alisema Cordeiro.

“Lakini asante kwa hii mbinu mpya, kweli wataendelea kuwepo Wajapani na Wakorea, kwa sababu wataishi milele na kubakia vijana.”

Gharama ya matibabu ya kuzuia uzee inalinganishwa na  ile ya  SimuJanja za karibuni.

“Mwanzoni, itakuwa ghali, lakini kwa soko shindani bei itapungua taratibu kwa sababu kitu kimnufaishacho kila mmoja,” Alisema Cordeiro.

“Teknolojia, ikiwa bado mpya, ni dhaifu na gharama sana, lakini hatimaye huwa ya kidemokrasia na kutawala na kuwa rahisi.”

Wahandisi wamesema kuwa tayari wamewekeza mbinu zao miaka 2 – kiharamu, lakini Colombia ambapo kuna taratibu chache zinazohusu uendeshaji genitiki.

Elisabeth Parrish, mgonjwa wao wa kwanza, 'alianza kuona dalili za kuzeeka na kuuliza kipi kingaliweza kufanyika ili kuzuuzuia'.

Matibabu yake ni 'hatari sana na haramu pia', Wood alieleza, lakini hivi sasa anaendelea vema, hayajatokea madhara yoyote yatokanayo na matibabu, na kiwango cha telomeres katika damu yake ni 'miaka 20 kiudogo zaidi ya kabla ya matibabu'.

“Nataka Hisapania iwe na  sehemu katika dunia ya hii mbinu na kuonesha kuwa sisi sio vichaa, ni vile watu bado hawawafahamu,” Wood alihitimisha.

Mwisho wa kifo "The Death of death" hatimaye kitachapishwa katika lugha nne kwa mara ta kwanza– Kihispania/Kihispaniola, Kingereza, Kireno na Kikorea – na mspato yote toka kwa mauzo yake yatawekezwa kwa  utafiti wa mwandishi.

 IMETAFSIRIWA NA Nascent Franzwa
nascentfrancium@yahoo.com
B.Sc Agriculture General
" Self-Proclaiming Extension Officer "