Monday, 11 July 2016

Masanja Mkandamizaji mbioni kuitwa baba



MASANJA MBIONI KUITWA BABA MZAZI KWA WANAWE

    
 Hii imetokea kwenye ibada katika kanisa la miito ya Baraka Jangwani Dsm

Mchekeshaji,Muhubiri na Mshereheshaji Masanja Mkandamizaji push and shadow stelingi.shinyanga vijijini amvisha pete mke wake mbele ya macho ya Mwakibolwa.
Huu ni mfano bora kwa vijana wengi wa kileo ambao wamekuwa wakiaminishana kuwa kwa sasa hakuna haja ya kuoa.............Nini maoni yako?????????????

Sunday, 10 July 2016

BAVICHA KWENDA DODOMA

MBOWE AWATULIZA VIJANA WA BAVICHA

 

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Freeman Aikael Mbowe leo Jumapili 10/06/2016(jana) amewataka vijana wa CHADEMA nchi nzima waliokuwa wamejiandaa kuelekea mjini Dodoma kwa ajili ya kulisaidia jeshi la Polisi kuwaambia wanachama wa CCM kutii tamko lililotolewa na Rais Dkt. John Magufuli ya kufuta shughuli zote za siasa ikiwemo mikutano ya hadhara, mikutano ya ndani, makongamano n.k kutokwenda tena Dodoma mpaka utaratibu mpya utakapotolewa.
Akiongea katika semina ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri wanaotokana na CHADEMA jijini Arusha leo, Mbowe ametumia fursa hiyo kulitaka Jeshi la polisi kuacha kupendelea Chama kimoja, na waelewe kwamba Rais ni mwanasiasa, amechaguliwa kupitia Chama cha siasa, shughuli anazozifanya ni za kisiasa, Waziri Mkuu,Wakuu wa mikoa, wakuu wa Wilaya nao wanafanya shughuli za siasa.
"Nawataka vijana wote nchi nzima waliokuwa wanajiandaa kuelekea Dodoma, waache kwenda mpaka watakapojulishwa utaratibu mwingine kutoka ndani ya chama, kwa sababu Polisi wanapanga kufanya jambo ovu, kwani wameanza kuwakamata viongozi wa BAVICHA, waliokuwa wapo Dodoma, amekamatwa Patrobas Katambi ambaye ni Mwenyekiti wa BAVICHA na Julius Mwita ambae ni Katibu wa BAVICHA Taifa, wamekutwa wakila chakula wakakamatwa, kwa sababu Bwana Katambi ni Mwanasheria alitaka kujua kosa lake, lakini walimpiga, hili ni jeshi gani la Polisi lisilotambua wajibu, kulinda raia na mali zao" amesema Mhe. Mbowe.
Sheria ya vyama vya siasa na Marekebisho yake yote, yanatambua haki za vyama vya siasa kufanya shughuli zake za siasa bila kuvunja Sheria, huku Jeshi la Polisi likitoa ulinzi huo ukiwa ni wajibu wake.
Mbowe amesisitiza kwamba hawataomba tena kibali kwa jeshi la Polisi wala mamlaka yeyote, lakini wanabuni njia nyingine ya kufanya siasa, kwa sababu siasa ni maisha ya kila siku.
Wanakataza shughuli za kisiasa kwa sababu hawataki kukosolewa, wakati kuna mambo mengi sana ya kuikosoa Serikali, Serikali isiyotaka kukosolewa sio sikivu kwa wananchi inawaongoza.
Mhe. Mbowe amesisitiza kuwa wataendelea kupagania haki ya Taifa hili mpaka haki itakapotendeka, shauri lililokuwa limefunguliwa jijini Mwanza kupinga zuio la mikutano ya hadhara na maandamano jijini Mwanza, hivyo shauri hilo limehamkshiwa Mahakama Kuu Dar es salaam kupinga zuio la mikutano ya hadhara, maandamano, na shughuli mbalimbali, yakiwemo makongamano, mikutano ya ndani ya vyama vya siasa n.k.
Akiongea katika Semina ya Mameya na Wenyeviti wa halmashauri zinazotokana na CHADEMA, Mbowe amewataka wahakikishe wananchi waliowachagua wanawatumikia ipasavyo, kuhakikisha huduma muhimu zinapatikana kwa wananchi, kama afya,elimu n.k, Mbowe amewataka viongozi hao wawe wabunifu zaidi katika kutatua matatizo ya Wananchi waonyoshe tofauti kwa sababu Wananchi wamewaamini.
"Kuna tatizo kubwa sana la ajira nchini, hakikisheni mnatengeneza fursa za kutosha ambazo zitawapa vijana na watu wote ajira, maisha yamekuwa magumu maradufu, kila kukicha bora ya jana, nyie kama viongozi wa maeneo yenu kaeni na wananchi wenu, mbuni fursa ambazo zitawafanya wananchi wenu waweze kujikwamua kiuchumi" Amesema.
Pia Mhe. Mbowe amewataka Viongozi hao kuacha kutoa pesa kwa vyama vya siasa, watu wa CCM kuwekewa mafuta na kupewa pesa kutoka Halmashauri, kuanzia sasa, Mhe. Mbowe amewataka viongozi hao kuwanyima, na wakiendelea atawaumbua, Halmashauri hazitakiwi kutoa pesa kwa vyama vya siasa, iwe CCM,CHADEMA, CUF n.k.
Katika semina hiyo ambayo imefungwa Rasmi na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Mhe. Freeman Mbowe, pia umefanyika uchaguzi ambapo Meya wa jiji la Arusha,amechaguliwa kuwa Mwenyekiti,Katibu wake ni Meya wa Manispaa ya Kinondoni,na Mnadhim amekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Tarime.
Viongozi hao watatu,wamekuwa Wajumbe wa Kamati Kuu.
Imetolewa Na: Kurugenzi Ya Habari Chadema



Ufaransa yaadhibiwa na Ureno

France Loses a Soccer Championship, but Achieves a Rare Unity

PARIS — Cristiano Ronaldo spends a lot of time alone. Alone on the wing, alone in his kitchen, alone in his thoughts, where, by his own admission, much of his focus is on whether he will again win the Ballon d’Or award — the world player-of-the-year honor, which, of course, is for a single, solitary superstar.
Ronaldo does not mind this (or, at least, he says he embraces it). Even by modern athletic standards, his entourage is necessarily small: his agent, his manager, a few close friends and his family. That is it. He often eats lunch by himself, often drives to practice by himself. Over the last 13 years, he has cultivated an image as someone who lives lavishly and luxuriously — estimates are that he is worth $320 million and so the pictures of him on a yacht are to be expected — yet also in relative quiet.
He has his 6-year-old son, Cristiano Jr. He has his agent and father or brother figure, Jorge Mendes. He has his soccer and his stardom and, depending on the particular parameters of the argument, his place on or near the top of the list of soccer’s greatest figures.
But here is the thing: Much of Ronaldo’s life is built upon his place at his club team, Real Madrid. This is not to say that Real Madrid is a house of loners or that there is no team spirit there; to the contrary, the club is strong and rich, and many of its supporters are passionate and devoted and true. But it is also undeniable that because of Madrid’s exorbitant resources — last year’s payroll was estimated at $180 million — there is a culture of stars, many of whom come and go. And Ronaldo, who has been the rare mainstay, is the brightest.
With Portugal’s national team, though, it is different. Ronaldo is still the biggest star, even more so than with Madrid, but the meaning of his presence, and the results, are not the same. On Sunday, Ronaldo will captain Portugal when it faces France in the final of the European Championships, the first time Portugal has been in a major final since it was stunned, on home soil, by Greece in the 2004 Euros.
Ronaldo was 19 then, a wunderkind who cried on the field after the final whistle. It was a brutal, bitter experience, but it did not stick to him, did not tarnish him. Neither did disappointing defeats in the semifinals of the 2006 World Cup or the 2012 Euros. In this era, results in international play are an additive to a player’s legacy, a bonus. Consider: Ronaldo and Lionel Messi are the near-universal choices as the best players in the game, yet neither has helped his country lift a significant trophy.
On Sunday at the Stade de France, that may change. Ronaldo has said, many times, that he craves a title for Portugal, that it is a dream for him. It is, presumably, a pure one, too: Winning will do little for Ronaldo financially. It will not make him more famous, either. Portugal has a population of a little more than 10 million; Ronaldo has six times that many Instagram followers.

Janga

PIGO KUBWA LATOKEA SUA

 
Picha ya Wardat Jampan
(marehemu)

Miezi michache baada ya mwanafunzi wa kiume wa mwaka pili chuo kikuu cha Sokoine katika kozi Sayansi ya chakula kupoteza maisha akiwa amelala maeneo ya mazimbu, pigo lingine limewapata tena wanafunzi wa chuoni hapo baada ya kumpoteza binti Wardat Jampan mwanafunzi wa ngazi ya cheti katika kozi ya IT......Binti Wardat aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya Mazimbu inayomilikiwa na Chuo hi alifikwa na umauti jioni ya tarehe 10 July 2017, ikiwa ni masaa machache kabla ya siku ya kuanza mitihani ya mwisho wa mwaka kufika......Mwili wa marehemu ulisafirishwa usiku wa siku hiyohiyo kweda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mazishi yatakayofanyika saa nne asubuhi kesho yake (Leo) tarehe 11/7/2016

Bwana alitwaa, Bwana ametwaa, jina la Bwana libarikiwe. Amina

Kuelekea UE

UE KULETA NEEMA TZ
Mitihani ya vyuo vikuu Tanzania maarufu kama UE inatarajiwa kuanza hapo kesho tarehe 11 Feb 2016 kwa vyuo kadhaa nchini ikiwepo IFM, SOKOINE pamoja UDSM.....Ni siku chache zimepita tangu nchi ya Rwanda iahidi kuisaidia Tanzania wataalamu wa IT ili kufanikisha zoezi la ukusaji wa mapato TZ....
Maramba media imefanikiwa kufanya mahojiano na wanafunzi kadhaa ambao wapo mwaka wa mwisho wa masomo yao na wametoa maoni yao juu Rwanda kuisaidia TZ wataalamu...Wanafunzi hao wamesema Tanzania ya sasa sio nchi yenye shida ya wataalamu bali inahitaji mifumo rafiki na viongozi imara kisiasa na wenye UZALENDO kwani miradi mingi iliyowahi kufeli nchini chanzo ni kutokuwepo viongozi makini pamoja na sababu nyingine ndogondogo....Aidha wamefika mbali zaidi kwa kuishauri serikali ya awamu ya 5 kuweka misingi imara na kuajiri vijana wa kutosha kati ya wahitimu wa mwaka huu katika sekta zote ili kuongeza ufanisi wa kasi ya ukuaji wa uchumi wa Taifa kwani vijana wanakuwa na uzalendo wa kazi zaidi ya wazoefu wa muda mrefu,pia ndi muda ambapo wataweza kuibadilisha elimu walioipata kwenda katika uzalishaji.........
Pamoja na hayo, pia wamesisitiza kuwa gharama za kuazima wataalamu nje ya nchi kwa kazi ambazo zaweza kufanywa na wataalamu wa hapahapa nchini ni kupoteza akiba ya fedha za kigeni ambazo zingeweza kufanya kazi nyingine za kimaendeleo.....
Kwakuwa huu ni wakati wa Tanzania iliyosubiriwa kwa miaka mingi, ni matumaini yetu sisi Watanzania kuwa serikali itayafanyia kazi mawazo hayo ya vijana wasomi wazalendo wa Kitanzania.....
Maramamedia inapenda kuwatakia wanafunzi wote wa SUA, IFM, UDSM pamoja na vyuo vyote vikuu Tanzania maandalizi mema ya mitihani yao,pia inawakumbusha wale wanaotegemea kuhitimu kuwa...."BAADA YA KUTUMIA GHARAMA KUJIENDELEZA KITAALUMA, SASA NI WAKATI WA TAIFA KUNEEMEKA KUPITIA UTAALAMU MLIOUPATA"